The House of Favourite Newspapers

MAMILIONI YA USAJILI YATUA YANGA

TETESI za kwamba muda wowote wiki hii, kipenzi cha wana Yanga Yusuf Manji atatangaza kurejea Jangwani zikaushie kwanza.

 

Kuna mkwanja umetua huo, unaambiwa mambo ni moto. Habari za uhakika ambazo Championi Jumatano imezipata ni kwamba kuna mkwanja viongozi waliuomba sehemu ambao unakadiriwa kuzidi Sh.Milioni 400, umetua kwenye akaunti ya klabu tayari na ndiyo unaowapa kiburi cha kuita wachezaji wakubwa mezani.

 

Tofauti na Simba ambao wamekuwa wakiwatangaza mastaa wao wapya kwa mbwembwe, Yanga hadi sasa haijaweka wazi imesajili nani licha kuhusishwa na wachezaji kadhaa wa ndani na nje ya nchi huku wakisisitiza mambo yao yanakwenda kimyakimya.

 

Awali ilikuwa ikielezwa kwamba mambo yanafanywa kimyakimya ili kuhofi a kuporwa wachezaji na wapinzani wao ambao ni Simba na Azam. Chanzo cha ndani cha uhakika kimesema kuwa Yanga sasa hawana tena shida ya fedha baada ya kiwango kikubwa walichokuwa wanakitegemea kwa ajili ya usajili kuingia kwenye akaunti yao lakini viongozi wamekubaliana itakuwa ni siri kubwa miongoni mwao lakini watakuja kuwaambia wanachama kwenye mkutano.

 

Chanzo hicho kimesema kuwa kuanzia leo au kesho timu hiyo ya Jangwani itaanza fujo za usajili na kila anayesubiri fedha yake Jangwani ataipata kwa kuwa mambo tayari ni safi . Kabla ya wachezaji wapya Yanga itawaongezea mikataba mastaa Kelvin Yondan, Hassan Kessy, Juma Abdul, Godfrey Mwashiuya, Andrew Vicent ‘Dante’, Beno Kakolanya, Matheo Antony, Juma Mahadhi na Mwinyi Haji.

 

Baada ya hapo ndiyo uongozi utaanza kazi ya kusajili majina mapema kwa kasi ya kimondo ili kukimbizana na muda kwani zimebaki siku chache sana kabla usajili haujafungwa na kama utafungwa hivi Yanga itakuwa na wachezaji saba tu halali.

 

“Uongozi ulikuwa ukisubiria pesa kutoka kwenye kampuni moja kubwa tu hapa nchini ili kufanya mazungumzo na wachezaji kwa ajili ya kuwaongezea mikataba, ambapo tayari pesa hizo zimeshaingia ndani ya wiki hii lakini bado hazijaanza kusoma, zikisoma tu basi watawaita wachezaji mmoja mmoja kwa lengo la kufanya nao mazungumzo na kusaini, yaani mtazikoma fujo za Yanga,” kilisema chanzo.

 

“Hakuna mchezaji hata mmoja ambaye amesajiliwa hadi sasa na majina yaliyokuwepo ni yaleyale ya wachezaji nane ambao hawajamaliza mikataba yao licha ya dirisha la usajili kutarajiwa kufungwa Julai 28, hivyo kuanzia wiki hii mwishoni kila kitu kitakuwa kwa spidi kubwa,” kilisema chanzo.

 

Championi Jumatano, linafahamu kuwa uongozi wa Yanga utaanza kuwapa mikataba mipya wachezaji wao ambao hawajamalizana nao akiwemo Kelvin Yondani baada ya hapo watawasajili Deus Kaseke, Mrisho Ngassa, Straika kutoka DC Motema Pembe, Jaff ary Mohammed ambaye amepitishwa na kocha, halafu ndiyo watafanya mazungumzo na Mnigeria.

Stori: Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Comments are closed.