The House of Favourite Newspapers

Man U Vs Barcelona ni vita ya matajiri

WANAONGOZA La Liga kwa tofauti ya pointi 11, wapo kwenye fainali ya Spanish Cup, vijana wa kocha Ernesto Valverde wanatarajiwa kuwa uwanjani leo Jumatano kuwavaa Manchester United, ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Hatua ya Robo Fainali. Vijana hao ni Barcelona ambao wakiongozwa na Lionel Messi watakuwa pale kwenye Uwanja wa Old Trafford kwa ajili ya kupepetana na Manchester United.

 

Messi amefunga mabao 33 hadi sasa katika La Liga, kwa kushirikiana na Luis Suarez kwa pamoja wamefunga mabao 14 katika mechi sita zilizopita (10 kwa Messi na manne kwa Suarez), lakini jumla katika michuano yote Messi hadi sasa amefunga mabao 43 katika mechi 40, bila kusahau kuwa ametoa asisti 17.

Kwa takwimu hizo pekee zinaonyesha jinsi ambavyo ushirikiano wa wawili hao ulivyo ni wa kiwango cha juu. Lakini wakati huohuo unatakiwa utambue kuwa klabu hizo zinatajwa kuwa moja ya klabu tajiri za soka na za michezo kwa jumla, pia zinaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi duniani kote, hivyo mchezo baina yao utakuwa unahusisha matajiri na mabilioni ya watu wanaozishabikia. Pamoja na takwimu hizo nzuri bado Kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer anayo nafasi ya kufanya kweli.

 

Moja ya udhaifu wa Barcelona ni katika kuzuia mashambulizi ya kushtukiza (counter-attacks), hivi karibuni walilazimishwa sare ya mabao 4-4 dhidi ya Villarreal, wapinzani wao wakitumia staili hiyohiyo ya kushambulia kwa kushtukiza.

 

Kiungo mkongwe wa Barcelona, Sergio Busquets naye ni kama kasi imeanza kupungua, anapokutana na wapinzani wanaotumia nguvu na wenye kasi amekuwa akipata tabu.

 

Upande wa ulinzi nako hakuko imara sana, wamekuwa wepesi wa kuruhusu bao hasa wanapopata presha kubwa. Kingine ni kuwa takwimu za Barcelona katika mechi za ugenini kwenye michuano ya Ulaya siyo nzuri.

 

Walitoka 0-0 dhidi ya Lyon, katika hatua ya mtoano, Barca haijapata nafasi ya kushinda mechi ya ugenini tangu walipoifunga Arsenal mabao 2-0, Februari 2016, baada ya hapo walifungwa na Atletico (2-0), Paris St Germain (4-0), Juventus (3-0) na Roma (3-0).
MANCHESTER

Comments are closed.