The House of Favourite Newspapers

MAN UTD YATUPWA NJE FA, YAPIGWA 2-1 NA WOLVES, CITY YAPETA

WAKATI Manchester United imetupwa nje ya michuano ya Kombe la FA, Manchester City iliweka hai matumaini yake ya kutwaa mataji manne msimu huu baada ya kutinga nusu fainali jana. Manchester United ilitupwa nje ya mic h u a n o hiyo baada ya k upigwa bao 2-0 na Wolverhampton Wanderers `Wolves’ kwenye mechi ya robo fainali iliyochezwa katika Uwanja wa Molineux.

 

Manchester City nao walifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuwashinda kwa taabu Swansea City kwenye mech i nyingine ya robo fainali ya michuano hiyo iliyochezwa katika Uwanja wa Liberty.

Wolv es ilijipatia bao lake la kwanza katika dakika ya 70 ya mchezo huo likipachikwa wavuni na Raul Jimenez. Jimenez alijaza wavuni mpira uliokuwa umewababatiza mabeki wa Manchester United kufuatia shuti lake mwenyewe.

 

Wolves iliongeza bao la pili katika dakika ya 76 likipachikwa na Diogo Jota, ambaye alikokota mpira kutoka katikati ya uwanja na kuachia shuti kali ambalo lilimshinda kipa wa Manchester United, Sergio Romero. Kipigo hicho hicho kilizima ndoto ya Manchester United ya kunyakua Kombe la FA.

Pia kilikuwa kipigo cha tatu kwa Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, ambaye tangu ameanza kuinoa timu hiyo mwezi Desemba, mwaka jana ameisimamia mechi 19, ambapo ameshinda 14, amepoteza tatu na ametoka sare mbili, Nayo Manchester City iliishinda Swansea kwa mbinde kwenye robo fainali nyingine ya Kombe la FA na kuendeleza vita yake ya kutwaa mataji manne ambapo ikiwa tayari ina Kombe la Carabao, ambapo pia inawania ubingwa wa Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Swansea ndio ilitangulia kufunga mabao mawili, ambapo bao la kwanza lilipachikwa kwa penalti na Matt Grimes katika dakika ya 20 wakati bao la pili likifungwa na Bersant Celina katika dakika ya 29.

 

Hata hivyo, Manchester City ilicharuka na kupata bao la kwanza kupitia kwa Bernado Silva kwenye dakika ya 69 wakati mabao mengine yakifungwa na Sergio Aguero kwenye dakika za 78 na 88. Mapema Watford ilitinga nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuiliza Crystal Palace mabao 2-1 wakati mechi nyingine ya robo fainali itapigwa leo kati ya Millwall na Brighton.

Comments are closed.