The House of Favourite Newspapers

Mane, Salah Wakodiwa Ndege Kwenda Ghana

Sadio Mane.

KLABU ya Liverpool imewakodia ndege mastaa wake wawili, Sadio Mane na Mohamed Salah ambao wanakwenda kushiriki utoaji wa Tuzo za Mchezaji Bora wa Afrika.

 

Wachezaji hao wanatarajiwa kuondoka kwenye klabu hiyo keshokutwa Alhamisi na kutarajiwa kurejea usiku huohuo nchini England.

Liverpool wametoa taarifa kuwa wachezaji hao watakodiwa ndege na ilikwenda nchini Ghana kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za utoaji wa tuzo hizo ambazo wote wawili wanashiriki.

Mohamed Salah

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema kuwa anaamini wachezaji hao wanaweza kwenda na kurejea England kucheza mchezo wa Kombe la FA, dhidi ya Everton, Ijumaa.

“Wataondoka hapa asubuhi na watarejea mara tu baada ya tuzo hizo kumalizika, hawatakuwa na muda wa kupoteza kwa kuwa wana mchezo Ijumaa,” ilisema taarifa kutoka Liverpool.

 

“Tumeandaa kila kitu vizuri, tuna wachezaji wawili kati ya watatu ambao wanawania tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Afrika, lazima tuwaonyeshe heshima.

“Sisi kwetu kila kitu kipo kwenye mpangilio mzuri sana na wa heshima kuwa kila mmoja ambaye tunafanya naye kazi,” alisema kocha wa Liverpool, Juggen Klopp.

 

Salah bado anasumbuliwa na majeraha ya nyonga ambayo yalimfanya aukose mchezo wa juzi dhidi ya Burnley na kocha huyo amesema kuwa kama atakuwa hawajapona hadi Ijumaa basi hatacheza mchezo dhidi ya Everton.

YANGA Yafunguka Ishu Nzima ya Chirwa Kukosekana Kikosini

 

Comments are closed.