The House of Favourite Newspapers

Beki: Yanga Nipeni Fedha Zangu Au Nisepe

Beki wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi.

BEKI wa kushoto wa Yanga, Haji Mwinyi ameibuka na kusema kuwa mipango yake kutaka kuondoa kwenye timu hiyo ipo palepale kwa kuwa hata yeye anawadai pesa nyingi Yanga na hajui atalipwa lini.

 

Mwinyi ameyasema hayo kufuatia dili lake la kutaka kujiunga na AFC Leopard likielekea kuyeyuka licha kuan­dika barua ya kuomba kuachwa baada ya kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mwinyi alisema hao­ni sababu ya uongozi wa timu hiyo kushindwa kumuachia kwa kuwa ameshawapa barua ya kuomba kuachwa licha ya ku­wadai pesa nyingi za mishahara pamoja ada ya usajili.

 

“Kiukweli mipango yangu ya kuondoka bado ipo kwa sababu hata kule Kenya usajili unafun­gwa Januari 15 na kikubwa ni ile timu kuweze kufika hapa wamalizane ili niondoke zangu.

 

“Nadhani hapa wao wame­kuwa wagumu kwa sababu ya mkataba wangu bado mrefu ila kama hawatotaka kuniruhusu itabidi wanilipe malimbikizo yangu maana nawadai pesa nyingi zikiwemo za ada ya usajili na sijui nitalipwa lini,” al­isema Mwinyi.

 

Ikumbukwe, uongozi wa Yanga kupitia katibu wa timu hiyo, Boniface Mk­wasa umeweka wazi suala la mchezaji huyo watakuwa tayari kumuachia kuon­doka iwapo AFC Leopard watafuata utaratibu wa kuwapelekea barua rasmi na siyo kutegemea simu.

Comments are closed.