The House of Favourite Newspapers

Manula, Kanoute kuikosa Wydad Casablanca Jumamosi Uwanja wa Mkapa

0
Aishi Manula.

KUNA kila dalili za nyota wawili tegemeo wa Simba, Aishi Manula na Sadio Kanoute kuikosa mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi hii dhidi ya Wydad Casablanca kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Manula yupo nje ya kikosi hicho akisumbuliwa na majeraha ya bega, wakati Kanoute anasumbuliwa na nyonga. Nyota hao pia waliukosa mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambao Simba ilishinda 2-0.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Manula na Kanoute hawatakuwa sehemu ya mchezo kufuatia kuwa na majeraha, hivyo kwa taarifa za madaktari tayari zipo wazi hawataiwahi Wydad hiyo Jumamosi.”

Spoti Xtra limezungumza na Meneja wa Idara ya Habari ya Simba, Ahmed Ally, ambapo amesema: “Ni kweli Kanoute na Manula walipata majeraha ambayo yaliwafanya kukosa mechi ya Yanga, hivyo kwa sasa tunasubiri ripoti ya madaktari ili tufahamu kama watakuwa sehemu ya mchezo ujao.”

STORI NA MUSA MATEJA

Leave A Reply