The House of Favourite Newspapers

Manula, Kanoute Wawakosa Biashara Leo

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amethibitisha kukosa huduma ya nyota wake watatu kwenye mchezo wa leo Ijumaa dhidi ya Biashara United utakaopigwa kwa Mkapa saa 1:00 usiku.

 

Pablo amesema atawakosa kipa Aishi Manula ambaye ana matatizo ya kifamilia, Sadio Kanoute (majeraha) na Taddeo Lwanga ambaye bado hajawa fiti.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa Pablo alifunguka: “Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Biashara baada ya kumaliza majukumu yetu kwenye mechi za kimataifa, tutaingia kwenye mchezo huu kwa kuwaheshimu kwani wamekuwa na mchezo mzuri dhidi ya timu kubwa ukizingatia walifanikiwa kutuzuia kwenye raundi ya kwanza.

“Vijana wapo tayari kwa ajili ya mchezo isipokuwa tutawakosa Aishi Manula ambaye amepata matatizo ya kifamilia, Sadio Kanoute alipata majeraha kwenye mchezo uliopita dhidi ya Berkane na Taddeo Lwanga ambaye bado hajawa fiti.”

Kwa upande wa Vivier Bahati, kocha mkuu wa Bisahara United alifunguka kuingia kwenye mchezo huo kwa tahadhari kubwa kwa kuwa anawafahamu Simba.

“Tunawaheshimu Simba hivyo ni lazima tuingie kwa tahadhari kubwa kwa kulinda na kushambulia kadiri tutakavyopata nafasi, hatupo kwenye nafasi nzuri katika msimamo hivyo tutaingia kwa tahadhari kubwa kama hatutapata alama tatu basi tupate alama moja ambayo itatusogeza hatua nyingine,” alisema Bahati.

 

Pia Pablo amethibitisha kurejea kwa viungo wake Rally Bwalya na Mzamiru Yassin ambao walikosekana kwenye mechi mbili za Kombe la Shirikisho kwa sababu ya matatizo ya kifamilia ambapo hawakuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri kwenda Niger na Morocco.

Waandishi: Hussein Msoleka, Marco Mzumbe na Mwanawahi Mpate

HALI ILIVYO MAHAKAMANI BAADA YA MBOWE KUACHIWA HURU…

Leave A Reply