The House of Favourite Newspapers

Mapacha Walioacha Kuzungumza Kwa Miaka 20 Wajinyonga

0
MAPACHA
Walipokuwa watoto..
MAPACHA
David (kushoto) na Paul wakiwa watu wazima.

 

MAPACHA wawili wa kiume, David na Paul Mann (55) ambao waliacha kuzungumza kwa miaka 20 baada ya kugombana kuhusiana na chakula cha aina ya pizza (aina ya mkate au chapati inayojazwa vikorombwezo mbalimbali ndani yake) walijiua mwaka huu kwa njia inayofanana lakini wakipishana miezi kadhaa tu.

Watu hao walikuwa ni wakazi wa Hampshire, Uingereza, wote wakiwa walipoteza mawasiliano na watoto wao na walitengana na wake zao kwa matatizo.

Paul alikutwa amejinyonga mwezi Agosti, ikiwa ni miezi mitatu baada ya David naye kujinyonga, yote hayo yakisemwa yalitokana na mifadhaiko hiyo ya kifamilia na kifedha.

Paul alikuwa amepoteza mawasiliano na mwanaye na akawa amedhamiria kurudisha uhusiano na David, lakini baada ya kusikia kwamba alikufa kwa kujinyonga, naye akaamua kufanya hivyo.

Ugomvi wa wawili hao ulianza siku ambayo walikuwa wanafanyiwa pati na wanaume wenzao kwa ajili ya matayarisho ya kuoa. Haikuelezwa vyema ni ugomvi gani uliowatenganisha wawili hao kutokana na pizza.


Maisha yao kwa jumla yalikuwa ni yenye matatizo ndani ya familia zao ambapo David aliyekuwa baba wa watoto watatu, aliwahi kujaribu kujinyonga kwa kunywa madawa yaliyozidi kipimo lakini alikwenda kunusurikia hospitali.

Isitoshe, aligunduika pia kuwa na deni la zaidi ya Paundi 80,000 alizokuwa amezilimbikiza kutokana na kodi.

NA WALUSANGA NDAKI/GPL

Leave A Reply