The House of Favourite Newspapers

Mapacha Wawili Wazaliwa Wakiwa Tofauti Kwenye Macho na Ngozi

0
Mapacha wasiofanana

MARA nyingi imezoeleka kuona mapacha wakifanana kila kitu kwa sababu ya kutoka kwenye yai moja lakini hii imekuwa ni tofauti sana kwa mama wa mapacha wawili, Chantelle Broughton ambaye alijifungua watoto wawili wenye jinsia, ngozi na macho tofauti.

 

Mama huyo mwenye umri wa miaka 29 amesema kwamba mapacha wake ni wakike na kiume na hawakuonekana tofauti sana wakati wa kuzaliwa lakini kadiri ya siku zilivyozidi kwenda ndipo tofauti zao zilipoanza kuonekana.

 

Chantelle amesema kuwa baada ya miezi kadhaa mtoto wa

wake wa kike alianza kubadilika ngozi na kuwa nyeusi na macho ya kuwa kahawia huku wakiume akibaki kuwa mweupe na macho kuwa ya kijani.

 

Mama huyo alijifungua mapacha wakike, Azirah na wakiume Ayon katika Hospitali ya Nottingham City na kufichua kuwa mara ya kwanza kuona mabadiliko hayo alishangaa sana na hakuamini.

Mama akiwa ameshika mapacha wasiofanana

Chantelle anaamini Azirah ana rangi nyeusi zaidi kwa sababu baba yao Ashton anaasili ya Jamaica na Scotland huku bibi yao akiwa ni Mnigeria.

 

Mama huyo amesema kuwa mapacha hao wa miezi minne, sasa wana haiba tofauti kabisa lakini familia na marafiki zake bado hawaamini kuhusu utofauti wa watoto hao.

Ameongeza kuwa mapacha hao huvutia watu wengi anapotoka nao nje huku wengine wakiamini kuwa huwenda wana baba tofauti.

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave A Reply