The House of Favourite Newspapers

Walimu Waliovujisha Mtihani Darasa la Saba Wapandishwa Kizimbani

0
Walimu saba na wafanyabiashara watatu wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kuvujisha mtihani wa Taifa wa Darasa la saba mwaka 2022.
Wakisomewa hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi Nassoro Katuga imewataja washtakiwa hao kuwa ni Theresia Chitanda, Elinami Sarakikya, Joyce Nkomola , Lloyd Mpande, Olomy Odongo, Docras Muro na Alcherous Malinzi na
Patrick Chawawa.
Hati hiyo ya mashtaka wamesomewa Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Pamela Mazengo, ambapo imedaiwa kuwa kati ya Oktoba 2 hadi 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam washtakiwa, walisambaza mtihani huo kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp na Telegram na kusababisha mtihani huo kuvuja  kwa watu ambao hawakuwa na mamlaka ya kuusimamia.
Imeelezwa kuwa katika tarehe hizo hizo Jijini Dar es Salaam mshitakiwa Malinzi alitengeneza nyaraka za uongo kuonesha kama mtihani wa Taifa wa Darasa la saba wa somo la uraia,  Maadili na Maarifa ya Jamii kuwa mitihani hiyo ni ya halali na umetolewa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), wakati akijua kuwa siyo kweli.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo  washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo ambapo miongoni mwa washtakiwa hao mshtakiwa mmoja tu ‘Mpande’ ndiye amefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyokuwa yamewekwa huku wengine wote wakirudishwa mahabusu.
Mahakama imewataka washtakiwa hao kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh. Milioni tano
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika hivyo wameiomba mahakama kuipangia tarehe nyingine kwa ajali ya kutajwa na imeahirishwa hadi Novemba 2 mwaka huu.
Leave A Reply