The House of Favourite Newspapers

Mapadri Jela Miaka 40 Kwa Ubakaji

Nicola Corradi (kulia- katika kiti cha walemavu  na Armando Gómez (wa tatu) na Horacio Corbacho (shati jeupe) wakiondoka mahakamani mjini Mendoza.

MAHAKAMA ya nchini Argentina imewahukumu makasisi (mapadri) wawili wa Kanisa Katoliki la Roma kifungo cha zaidi ya miaka 40 jela kwa kuwanyanyasa kingono watoto wenye ulemavu wa kusikia katika shule ya kanisa.

Makasisi hao ambao ni Horacio Corbacho (59) raia ya Argentina na Nicola Corradi (82) raia wa Italia walipatikana na hatia ya kubaka na unyanyasaji katika shule ya Kikatoliki iliyopo katika jimbo la Mendoza kuanzia mwaka 2004 hadi 2016.

Makasisi hao hawawezi kukata rufaa juu ya uamuzi wa mahakama kwa mujibu wa sheria za Argentina kuhusu makosa hayo.

Ndugu wa waathiriwa wakiangua kilio na kukumbatiana mahakamani

Comments are closed.