The House of Favourite Newspapers

Yanga Kukipiga na Namungo FC Leo, Kombe la FA

Kikosi cha timu ya Yanga.

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amewaambia mashabiki kwamba roho ya timu hiyo ipo kwenye michuano ya FA na leo watakinukisha dhidi ya Namungo FC mkoani Lindi.

 

Zahera amesisitiza kwamba leo watajitolea kwa nguvu zote zaidi ya walivyofanya kwenye mechi ya Mbao walipovunja mwiko.

 

“Roho yetu yote ipo kwenye haya mashindano ya FA kwa vile ndiyo yanayoweza kutupatia nafasi ya kushiriki kombe la Shirikisho mwakani. “Itakuwa ni mechi ngumu sana na tutapambana kwa nguvu kwa tutajitolea sana kama tulivyofanya dhidi ya Mbao tukafuta
historia kwenye uwanja wao.

 

Tutaishinda Namungo,” alisema Zahera ambaye makazi yake yapo Ufaransa lakini amekulia DR Congo. Namungo itakuwa ikiwatumia wachezaji wengi chipukizi ambao kwa wiki kadhaa walikuwa kambini wakijinoa kwa nguvu zote huku morali yao ikionekana kuwa juu.

 

Kocha wa Namungo, Bakari Malima amesisitiza kwamba hawaingii uwanjani kwa kuangalia jina la timu wanayokwenda kucheza nayo bali umuhimu wa mchezo huo kwani wanataka kuweka rekodi. Yanga au Namungo atakayevuka kwenye mchezo huo ataingia robo fainali. Yanga imepania kushinda FA kutokana na ushindani mkubwa uliopo kwenye Ligi Kuu ambapo kuna nafasi moja tu ya kufuzu Afrika.

Comments are closed.