The House of Favourite Newspapers

Mapigano Yazuka Tena Sudan Kusini

0

Sudan Kusini (1)

Leonard Msigwa na Mtandao

Mapigano yamezuka tena baina ya pande hasimu nchini Sudan Kusini.

Kuna hofu kuwa Sudan Kusini huenda ikatumbukia tena kwenye vita vya kiraia.

Walioshuhudia wanasema wamesikia milio ya risasi katika mji muhimu wa Yei, kusini magharibi mwa Juba, kwenye barabara inayounganisha Juba na taifa jirani la Uganda.

Vikosi vitiifu kwa Makamu wa Rais, Riek Machar, vinasema kwamba vikosi vya serikali viliwashambulia katika maeneo yao siku ya Jumamosi.

Mwezi uliopita vikosi vitiifu kwa Rais Salva Kiir na Riek Machar vilikabiliana mjini Juba, katika makabiliano yaliyoifanya UN kutuma walinda amani 400 zaidi nchini humo.

Sudan Kusini (3)

Rais Salva Kiir na Riek Machar wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya amani.

Hata hivyo Bw. Kiir amesema hataruhusu Umoja wa Mataifa kuchukua udhibiti wa nchi yake na hatashirikiana tena na umoja huo.

Kila upande mara kwa mara hutupiana lawama kwa kuanzisha vita.

Sudan Kusini (2)

Uhasama wa kisiasa baina bwana Kiir na bwana Machar uliingia dosari baada ya kuzuka kwa mapigano  kati yao mwaka 2013 huku kila mmoja akiulumu upande mwingine.

Wawili hao walitia saini mkataba wa amani mwaka 2015, japo mapigano ya mara kwa mara yamekuwa yakiendelea baina ya pande hasimu.

Sudan Kusini (4)

Raia wa Sudan Kusini waliokimbia nchi hiyo.

Zaidi ya raia 100,000 wa Sudan Kusini kwa sasa wamekimbilia katika nchi jirani kufuatia mapigano ya hivi karibuni, shirika la la wakimbizi la Umoja wa Mataifa limedhibitisha.

 

Leave A Reply