The House of Favourite Newspapers

MAPINDUZI QUEEN WATAFUTA MPENYO KWA YANGA PRINCESS

UONGOZI wa kikosi cha Mapinduzi Queens kinachoshiriki Ligi ya Wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League umepania kupata mpenyo leo kupitia kwa Yanga Princess katika mchezo utakaochezwa leo Uwanja wa Karume.

 

Ofisa Habari wa Mapinduzi Queens Njenje Barnabas amesema wanatambua kwamba timu yao haina matokeo mazuri Ila leo watapambana kupata matokeo na kuwaomba mashabiki wajitokeze Kwa winging.

” Tunawaomba mashabiki wajitokeze Kwa wingi katika mchezo wetu wa leo dhidi ya Yanga Princess tunatambua ugumu iliopo Ila tutapambama kupata matokeo chanya.

 

“Kwa sasa timu haina matokeo mazuri ila twawaomba mashabik wetu wazidi kutusapoti kwani mambo mazuri yanakuja na tutafanya Mapinduzi ya kweli,” alisema.

Mapinduzi Queens wamecheza michezo nane na mpaka sasa wanapointi mbili wakiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi ya Wanawake Tanzania.

Comments are closed.