The House of Favourite Newspapers

MARADONA ATAKA KUMKATA KICHWA MPENZI WAKE!

BUENOS AIRES, Argentina: GWIJI wa soka nchini Argentina, Diego Maradona (58), kwa sasa yeye na mpenzi wake wa zamani ni paka na panya, lakini ametoa kali baada ya kutamka kuwa kuna wakati nusura amkate kichwa mrembo huyo.

 

Maradona, hivi ka­ribuni alitengana na Rocio Oliva, 28, na alikuwa amemzidi mi­aka 30 mrembo huyo.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio nchini Ar­gentina, Marado­na alisema: “Mimi siyo mpigaji wa mke, lakini yule nilitaka kumkata kichwa.

 

“Alisaini maku­baliano kwamba hatazungum­za chochote. Hizo bata ana­zokula kwenye mapumziko yake, anafanya hivyo kwa pesa zangu. Sasa yupo nje kabisa ya maisha yangu.”

Wawili hao wal­imwagana hivi kar­ibuni, baada ya miaka sita pamoja. Mara­dona amesema atai­chukua nyumba aliy­ompa mrembo huyo jijini Buenos Aires.

 

“Nyumba niliy­owapa familia yake ni yangu, nakwenda kuichukua. Samahani kama hawajui kum­tunza mtoto wao. Mimi siyo Father Krismasi ambaye nazunguka mtaani kuwauliza watu wa­nahitaji nini. Nafanya kazi kama mtu yeyote yule duniani ana­vyofanya.”

Maradona alionge­za kuwa Oliva hayupo vizuri kichwani, na penzi lao limekufa.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.