The House of Favourite Newspapers

Marekani: Waliofariki kwa Moto wa Msituni ‘Camp Fires’ Wafikia 42

IDADI ya watu waliofariki kutokana moto wa msituni katika maeneo mawili ya jiji la Los Angeles,  Jimbo la California nchini Marekani imefikia 42 hivyo kuweka rekodi mpya ya vifo kutokana na moto katika jimbo hilo.

Waliofariki walikutwa kwenye magari baada ya kukumbwa na moto mkubwa uliokuwa unasambaa kwa kasi, wengine walifariki wakiwa majumbani mwao.

Takribani watu 228 hawajulikani walipo, majengo zaidi ya 7,200 yameharibiwa huku mengine 15,500 yakiwa hatarini kuharibiwa na watu 250,000 wamelazimika kukimbia makazi yao.

Moto huo mkali uliopewa jina la Camp Fires ulianza Kaskazini mwa jimbo hilo na kuteketeza kabisa Mji wa Paradise.

Gavana wa Jimbo hilo, Jerry Brown,  amesema,  “Hatujui sababu za moto huo ila Mji wa Paradise ulijitayarisha vya kutosha kukabiliana na hali mbaya ya hewa ya ukame na upepo mkali.”

Inasemekana huenda chanzo chake kikawa ni shughuli za kibinadamu kama kuchoma moto ndizo zimesababisha moto huo kusambaa na kuwa mkuwa.

Moto huo ambao ulianza usiku wa Jumapili, mpaka sasa umeteketeza maeneo yenye ukubwa wa ekari zaidi 85,500 na kwamba umesambazwa zaidi na upepo mkali.

Comments are closed.