The House of Favourite Newspapers

Marekani Yatoa Onyo Kali kwa Korea Kaskazini Kuhusu Jaribio la Nyuklia

0
Naibu Katibu Mkuu wa Ikulu ya White House Wendy Sherman akiwa pamoja na mwenzie wa Korea Kusini Cho Hyun-dong jijini Seoul

SERIKALI ya Marekani kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wa Ikulu ya White House Wendy Sherman imeionya Pyongyang kuhusu jaribio lake la bomu la Nyuklia kuwa kwa kufanya hivyo ni kukuika sheria na kanuni za Umoja wa Maitaifa kuhusu usalama na kutailazimisha Marekani, Korea Kusini na Dunia kwa ujumla kujibu mapigo.

 

Sherman amenukuliwa akisema:

“Jaribio lolote lile la Nyuklia litakuwa ni ukiukwaji wa Sheria za Umoja wa Mataifa za Baraza la Usalama, kutakuwa na muitikio wa lazima na haraka kuhusu jaribio hilo.” Alisema Sherman wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye kikao na mwenzie wa Korea Kusini Cho Hyun-dong jijini Seoul.

 

Sherman aliongeza kwa kusema Dunia itajibu mapigo kwa namna sahihi kabisa tupo vizuri na tumejipanga.

 

Kumekuwa na wasiwasi kutokana na Koreza Kaskazini ambayo tayari imeshafanya majaribio ya makombora mbalimbali mwaka huu uwa ipo katika mchakato wa kufanya jaribio la mabomu ya Nyuklia tangu ifanye hivyo mara ya mwisho mwaka 2017.

Eneo la Mtungi wa Nyuklia la Yongbyon lililopo nchini Korea Kaskazini

Jana Jumatatu Korea Kusini na Marekani zilirusha makombora nane angani kuelekea Mashariki mwa pwani ya Korea Kusini ikiwa ni siku moja tu baada ya Pyongyang kurusha makombora ya masafa mafupi.

 

Wakala wa Kimataifa wa nguvu ya Atomi (IAEA) Imetoa taarifa ikidai kuwa Korea Kaskazini imetanua miundombinu yake ya kuimarisha eneo la kutengeneza mabomu ya Nyuklia la Yongbyon.

 

 

Leave A Reply