The House of Favourite Newspapers

MARIA NA CONSOLATA WALIVYOPENDANA HADI KABURINI – VIDEO

 

WATOTO mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (20) waliofariki Jumamosi iliyopita Juni 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wataendelea kukumbukwa na maelfu ya Watanzania kwa kuweza kuyakubali maumbile yao waliyokuwa nayo na kuvumilia maisha yao mpaka kufikia hatua ya kufariki wakiwa katika mwili mmoja.

 

Novemba 19, 1997, familia ya Alfred Mwakiuki na Naomi Mshumbusi ilifanikiwa kupata watoto mapacha ambao ni Maria na Consolata lakini hawakuwa mapacha wa kawaida kama ilivyozoeleka, walikuwa wameungana na kwa wakati huo hapakuwepo na uwezekano wa kuwatenganisha.

 

 

Akizungumza wakati wa kutoa salamu za kuaga miili ya mapacha hao Askofu Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma amesema vifo vya mapacha hao vinafaa kutumiwa na Watanzania kukumbushana wajibu wao kwa watu wenye ulemavu.

Mbali na Askofu Maluma, Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza amesema mkoa huo umepata pigo kubwa la kuondokewa na pacha hao waliokuwa na upendo wa dhati na wenye kujitambua.

 

“Mkoa wa Iringa tumepata mtihani wa kuondokewa na watoto waliokuwa na upendo sana, najua kwa jinsi gani tulivyokuwa tunawapenda lakini Mungu amewapenda zaidi. Maria na Consolata walijitambua na wakakubali maumbile waliokuwa nayo halafu wakajiamini ndio maana waliweza kusoma kwa bidii na kufiki hatua ya chuo kikuu”, amesema Masenza.

 

 

Masenza amesema “Niwaombe wazazi kwamba serikali ipo tayari kuwasaidia watoto wenye ulemavu hakuna haja ya kuwaficha, waacheni watoto waje maana neema yao ipo. Kuwaficha huko ni kutenda dhambi”.

 

Maria na Consolata walizaliwa Novemba 19, mwaka 1997 ambao enzi za uhai wao walikataa kutenganishwa miili yao na kupelekea leo hii kuzikwa kwenye jeneza moja litakalokuwa na misalaba miwili  katika makaburi ya viongozi wa dini yaliyopo Tosamaganga mkoani humo.

 

Misa ya Kuwaombea Marehemu Maria na Consolata Kabla ya Mazishi – Video

LIVE IRINGA: Mazishi ya Maria na Consolata Leo

Comments are closed.