KAMPUNI ya mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ wikiendi iliyopita iligeuka gumzo baada ya Masanja kuonekana akiwa na wahudumu wake akiwa amevalia vazi la kuuzia vyakula lenye maandishi ya ’Masanja Wali Nyama’.
Msanii huyo alionekana katika hafla fupi ya semina iliyofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) iliyokuwa imeandaliwa na wahamasishaji maarufu Antony Luvanda na Dk. Chris Mauki ambapo Masanja alikuwa akihudumia wageni waalikwa sambamba na mkewe Monica aliyefunga naye ndoa hivi karibuni.
Mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya‘Masanja Mkandamizaji’ akitokelezea na vazi lake lililoandikwa ‘Masanja Wali Nyama’.
Mke wa Masanja aitwaye Monica akiwa na wahudumu wengine wakionesha vyakula wanavyoviuza.
Mke wa Masanja (kulia aliyeko mbele) akinyoosha kidole.
Masanja akiwa na mkewe Monica na nyuma yao ni baadhi ya vyakula wanavyoviuza.
Wakibeba vyakula hivyo.
Wakiendelea kutoa huduma.
Stori: Denis Mtima / GPL








