The House of Favourite Newspapers

MASHABIKI WATAKA DUDU BAYA ACHUKULIWE HATUA

WIKI iliyopita kwenye safu hii tulimuweka mwanamuziki wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ ambaye hivi karibuni baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kutangaza kuwasaka wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja ‘mashoga’ na kuwataka watu wamtumie majina yao, yeye aliwataja waandishi wa habari na watangazaji mbalimbali ambao hapa hatuoni sababu ya Mashabiki na wasomaji wengi walituma maoni yao kuhusiana na jambo hilo alilolifanya Dudu Baya, kama yanavyosomeka hapa chini:

 

DUDU Baya ni mshamba angejaribu kugeuza upande wa pili wa shilingi akumbuke kuwa hao waandishi na watangazaji ndiyo waliompaisha mpaka akajulikana, hana fadhila huyo. Cecy -Pangani.

***

DUDU Baya alivyofanya siyo sawa kwa sababu hana uhakika na hajawahi kuwaona wakifanya uchafu huo. Da Mbeho – Kibaigwa.

***

DUDU Baya hakufanya poa kuwadhalilisha watu na familia zao si jambo la kiungwana. Kama anatafuta kiki afanye muziki mzuri kama wenzake akina Diamond na Kiba apate pesa na siyo kudhalilisha watu kwa sifa za kijinga hata kama anawajua itamsaidia nini? Patrick Mtiifu – Dar.

***

DUDU Baya nakupongeza kwa kuwataja hao wanaohusika na ushoga na wanaolea mashoga,

endelea kutumbua majipu. Mwamvua Telacky-Moshi.

***

HUYO Dudu Baya atakuwa na matatizo, amewadhalilisha sana wenzake. Neema -Iringa.

***

UHURU wa mtu kutoa maoni au kuchangia chochote ni haki kwa kila binadamu isipokuwa faragha ya mtu mwingine si vyema kuitangaza hadharani bila ridhaa ya mtu husika, ndugu yetu labda alijua yupo sahihi kimtazamo wake lakini hakujua kwa upande mwingine kuwa anakosea. John -Makambako.

***

ALICHOKIFANYA Dudu Baya ni sawa kabisa kwa sababu kwanza ametekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Dar. Pili hao wanaotaka ushahidi ya kwamba wao siyo mashoga wampeleke mahakamani, binafsi naunga mkono kampeni ya kutokomeza mashoga Dar na Tanzania nzima ee Mwenyezi Mungu mbariki Makonda ili aongeze nguvu zaidi katika mapambano hayo na umpe afya Dudu Baya aweze kuwasema na wengine hadharani. Mjomba Ramso- Kilosa.

***

Tumsamehe Dudu Baya kwa hili nadhani kisaikolojia hayupo sawa kwa sasa. Ramadhan Hamady -Dar.

***

Alivyofanya Dudu Baya kiukweli siyo vizuri halafu yeye ni msanii mkubwa sasa kutafuta sifa za kijinga kwa kuwadhalilisha watu huo ni ushamba uliopitiliza, naomba wahusika wamchukulie hatua ili authibitishie umma maneno aliyoyatamka. Najma – Kibamba.

***

Alichofanya Dudu Baya ‘Konki, Konki, Konki masta’ siyo kizuri ila tatizo lipo kwa aliyetoa amri ya kufichua mashoga. Muddy Madiley – Dar.

***

Dudu baya hana uhakika na hao aliowataja. Si busara kuanza kuchafuana, haya mambo yasituwekee uhasama sisi kwa sisi, usimtaje mtu kwa kumuhisi.

Majuto Magazeti -Iringa.

***

Alichokifanya Dudu Baya naweza kukubaliana naye, ingawa hakuweka ushahidi wa kutosha dhidi yao hao waandishi na wanahabari kwa kuwashuku ushoga. Naweza kusema matendo ya waandishi hao yamechangia kuhisiwa vibaya; we mwanaume kutoboa masikio, kuvaa hereni, kusuka, kuvaa cheni na kadhalika ni dalili mbaya. Mbisso -Tabora.

Comments are closed.