The House of Favourite Newspapers

MAJANGA YA WEMA YAMKUTA SASHA!

UPEPO mbaya kwa mastaa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Video Queen Bongo, Sasha Kassim kukutwa na majanga ya kutapeliwa kama ilivyomtokea muigizaji Wema Sepetu, Risasi Mchanganyiko lina ‘full’ stori.

Wema aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na jamaa aliyefahamika kwa jina la Patrick Christopher ‘PCK’ ambaye baadaye ilielezwa kuwa ‘alimpiga’ takriban shilingi milioni 40 baada ya kumrubuni kuwa atafanya naye biashara.

 

MAJANGA YA SASHA

Chanzo makini kililinyetishia Risasi Mchanganyiko kuwa, kwa sasa Sasha hana maelewano mazuri na baba yake mzazi kwani alimpatia shilingi milioni 10 ili afanye biashara lakini yeye akampa mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Balele mkazi wa Geita aliyekuwa akimdanganya kuwa ni tajiri wa madini na atamsaidia kuwa mfanyabiashara mkubwa wa dhahabu.

“Hivi mnajua majanga yaliyomkuta mwanadada Wema Sepetu ya kutapeliwa na bwana yamehamia kwa Sasha? Jamaa kamrubuni, akajifanya babybaby, Sasha akakolea kwa mahaba, akampa mtonyo, akapigwa.

“Ukimuona hana raha kabisa, huyo jamaa awali alianza uhusiano naye akimdanganya kuwa ni tajiri wa huko Geita, walipokaa kwenye uhusiano wa miezi sita tu akamtapeli pesa ambazo amepewa na baba yake.

“Huwezi kuamini yule baba (Balele) kwa sasa anamkwepa Sasha, ameshambadilishia namba za simu kama tatu hivi anafanya kumpiga tarehe tu lakini pesa ndiyo kapigwa hivyo na baba yake hataki kumsikia,” kilisema chanzo.

 

SASHA ATHIBITISHA

Baada ya kupata ubuyu huu Risasi Mchanganyiko lilimsaka Sasha ambaye alikiri kupatwa na majanga hayo na kudai kuwa kinachomuuma ni baba yake ambaye alimuamini kuwa atafanya biashara kumbe ameishia kutapeliwa.

Mrembo huyo alisema, amechanganyikiwa na hajui la kufanya kwani mwanaume huyo alimuamini sana akijua kweli ni tajiri wa madini lakini mwisho wa siku amemtapeli fedha zake wakati alipokuwa kwenye dimbwi la mahaba.

 

“Sina la kusema nimeingizwa mjini, kweli wanaume ukiwaamini wakati mwingine wanaweza kukufanya chizi, mwanaume huyu nilimuamini kwa sababu tuliingia kwenye uhusiano kumbe ni tapeli mkubwa,” alisema Sasha.

AELEZA ALIVYOMPA FEDHA

Sasha anadai kuwa alikutana na Balele kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza akamuomba wawe marafiki, baadaye akamhitaji awe zaidi ya rafiki kwake (mpenzi) ambapo alimuomba muda afikirie lakini alikuwa akitoka naye na muda mwingi walikuwa pamoja kama marafiki wa kawaida.

“Siku moja aliniambia kuwa ana biashara ya madini anaifanya huko Geita nitafute pesa aniunganishe, nami nilikuwa natamani sana kuuza dhahabu nikamuomba baba yangu shilingi milioni 10 akanipa nikampatia ili aniletee mzigo ndiyo mpaka leo ananizungusha nimechoka hata sijui nitafanya nini,” alisema.

 

Alipoulizwa kama amelifikisha suala hilo polisi, Sasha alisema amebaki njia panda sababu fedha hizo alimkabidhi bila maandishi yoyote licha ya kuwa ana ushahidi wa meseji walizokuwa wakiwasiliana wakati akimdai fedha zake.

 

HUYU HAPA BALALE

Baada ya kuzungumza na Sasha anadai kuwa alikutana na Balele kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza akamuomba wawe marafiki, baadaye akamhitaji awe zaidi ya rafiki kwake (mpenzi) ambapo alimuomba muda afikirie lakini alikuwa akitoka naye na muda mwingi walikuwa pamoja kama marafiki wa kawaida.

 

“Siku moja aliniambia kuwa ana biashara ya madini anaifanya huko Geita nitafute pesa aniunganishe, nami nilikuwa natamani sana kuuza dhahabu nikamuomba baba yangu shilingi milioni 10 akanipa nikampatia ili aniletee mzigo ndiyo mpaka leo ananizungusha nimechoka hata sijui nitafanya nini,” alisema.

 

Alipoulizwa kama amelifikisha suala hilo polisi, Sasha alisema amebaki njia panda sababu fedha hizo alimkabidhi bila maandishi yoyote licha ya kuwa ana ushahidi wa meseji walizokuwa wakiwasiliana wakati akimdai fedha zake.

 

HUYU HAPA BALALE

Baada ya kuzungumza na Sasha gazeti hili lilimsaka Balale kwa njia ya simu ambapo alipokea na aliposomewa mashtaka yake alisikiliza kisha alikata simu.

 

TUJIKUMBUSHE

Kwa wafuatiliaji wa habari za mastaa, sakata hili ni sawa na lile lililomtokea Wema hivi karibuni. Bi dada huyo aliingia kwenye matatizo na mpaka sasa ana kesi mahakamani ya kupiga picha chafu na mpenzi wake, Patrick Christopher ‘PCK’.

 

Mbali na picha hizo, ilielezwa kuwa PCK alimtapeli Wema takriban shilingi milioni 40 alizolipwa za filamu yake mpya ya D.A.D aliyoizindua hivi karibuni kitendo ambacho naye kilimchanganya sana kwani alikutana na bwana huyo na kumuamini lakini mwisho wa siku akamuingiza matatizoni.

 

FUNDISHO

Mastaa wa kike wana jambo la kujifunza kutokana na sakata la utapeli huu wa wanaume ambao wanaingia kwa gia ya kujifanya wapenzi kisha baadaye wanajifanya wanataka kufanya baishara na matokeo yake wanawatapeli-Mhariri.

Stori:MWANDISHI WETU, RISASI MCHANGANYIKO

Comments are closed.