The House of Favourite Newspapers

Mashahidi 15 Wadsubiriwa Mahakamani Kesi ya Idris Sultan

0

UPANDE wa mashitaka unatarajiwa kuita mashahidi 15 na vielelezo mbalimbali wakati wa usikilizwaji wa kesi inayomkabili mchekeshaji Idriss Sultan na mwenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.

 

Idris anakabiliwa na shitaka la kushindwa kusajili laini ya simu iliyokuwa ikitumiwa na mtu mwingine. Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Inocent Maiga anayekabiliwa na kosa la kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki wa laini ya simu hiyo.

 

Washitakiwa hao leo, Alhamisi 9, 2020,  wamesomewa hoja za awali mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashidi Chaungu, ambapo waliyakana mashitaka hayo, isipokuwa majina yao, anwani zao na mashitaka yanayowakabili mahakamani hapo. Kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa Agosti 5 mwaka huu.

Leave A Reply