The House of Favourite Newspapers

Masharti ya mastaa wapya yamshtua Zahera

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema anaogopa kufanya mazungumzo rasmi na mastaa wapya watatu anaowataka kwa vile anaogopa masharti yao na hana hata senti mfukoni.

 

Zahera ameliambia Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili kwamba wachezaji hao wana masharti mengi ya uhamisho na aina ya mikataba yao inahitaji fedha ambazo kwa hali halisi Yanga haina.

 

Kocha huyo anataka winga kutoka Ghana pamoja na straika na kiungo kutoka DR Congo. Bosi huyo alisikitikia hali mbaya ya uchumi inayoendelea ndani ya Yanga ambayo imefanya mpaka wachezaji Kelvin Yondani na Beno Kakolanya kugoma kwenda Shinyanga kucheza na Mwadui FC wakishinikiza malipo yao.

 

“Kupata mchezaji mpya lazima ufanye uhamisho, lazima ukae nae mjadiliane mshahara wake atalipwaje na hata mkataba wake utakuwa wa aina gani,”alifafanua Zahera ingawa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omary Kaaya alizishangaa tuhuma hizo jana akidai kwamba hawajakaa na kocha tangu atoke kwenye timu ya Taifa.

 

“Siwezi kufanya mazungumzo kwavile sijaona kiongozi yoyote yule aliyeniambia hayo masharti ya usajili tutayafanya namna gani. Spoti Xtra linajua kwamba viongozi wa kamati ya usajili wa Yanga wanaendelea kusajili kimyakimya na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji aliwapa masharti kwamba wamvumilie mpaka sakata la uchaguzi lipite ndipo atakapotoa fungu la kusajili kwavile bado muda utakuwepo.

 

Yanga wamefanya mazungumzo na beki wa Rayon ya Rwanda, Abdul Rwatubyaye na kumwambia asubiri kidogo.

MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM.

KISHINDO Cha ujio mpya wa HABARI ZA MICHEZO Global TV Online

Comments are closed.