The House of Favourite Newspapers

Mashindano Wanaume Kubeba Wake Zao; Vicheko Mtupu

Mashindano ya Dunia ya Wanaume kuwabeba wake zao yamefanyika nchini Finland ikiwa ni kwa mwaka wa 23 mfululizo.

 

Mashindano hayo ambayo yamefanyika katika mji mdogo wa Sonkajarvi ambao una wakazi takribani 4,200, yaliwahusisha wanaume ambao waliwabeba wake zao mabegani na kukimbia nao kwa mita kadhaa na kuhudhuriwa na mamia ya wageni kutoka sehemu  mbalimbali.

Jumla ya familia (mke na mume) 53 zilishiriki katika shindano hilo ambalo lilishirikisha nchi 13 zikiwemo Marekani, Uingereza, Estonia, Sweden na Lithuania.

Wazo la kuanzisha shindano hilo lililetwa mnamo karne ya 19 na Ronkainen the Robber ambaye aliwashawishi vijana wenzake kubeba kati ya gunia la mbegu ama kumbeba nguruwe na kukimbia naye.

Shindano hilo lililohusisha pia washiriki katika kukimbia na kuruka vikwazo mbalimbali, lilishuhudia  washindi wakiwa ni  Vytautas Kirkliauskas na Neringa Kirkliauskiene raia wa Lithuania.

“Nafikiri kwa sababu tuna miezi mitatu pekee ya kuona mwanga tunahitaji kuwa na mashindano kama haya katika kipindi hiki na tunahitaji kumuonyesha kila mmoja uwezo wetuamesema  mmoja wa washiriki wa shindano hilo.

Finland ni nchi ambayo ina baridi kali, jua huonekana kwa miezi mitatu pekee katika mwaka mzima na katika sehemu za kaskazini jua huzama kwa siku 73 mfululizo bila kuchomoza katika kipindi cha kiangazi na huchomoza kwa siku 51 bila kuzama katika kipindi cha masika.

Comments are closed.