The House of Favourite Newspapers

Saa 24 Baada ya Hierro Kusepa, Enrique Atangazwa Kocha Hispania

ALIYEKUWA kocha wa klabu ya Barcelona ya Hispania, Luis Enrique, ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Hispania baada ya nchi hiyo kung’olewa katika Kombe la Dunia wakati wa kutafuta 60 bora katika michuano inayoendelea nchini Russia.

 

Kwa mujibu wa mkataba, Enrique ataishika nafasi hiyo kwa miaka miwili. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48, anachukua nafasi ya Hierro aliyepewa jukumu hilo saa 48 kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia Hispania ilipocheza na Ureno.

 

Kocha wa awali, Julen Lopetegui,  alifukuzwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia baada ya kukubali kuwa kocha wa klabu ya Real Madrid, na kumwacha aliyekuwa mkurugenzi wa michezo,  Fernando Hierro, kukaimu nafasi hiyo.

 

Enrique aliondoka Barcelona mwishoni mwa msimu wa 2016/17 baada ya kuitumikia miaka mitatu na baadaye kuzitumikia klabu za Chelsea na Arsena.

Comments are closed.