Maskini… Snura alizwa na mwanaye

snura-1IMELDA  MTEMA, Gazeti la Risasi Jumamosi, Toleo la Jan 14, 2017

MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara, Snura Mushi, amefunguka kuwa amekuwa akilizwa kila mara na mtoto wake wa kwanza Talha, kutokana na maneno anayomueleza kwa kitendo cha baba yake kutompa huduma yoyote.

Akizungumza na RISASI JUMAMOSI, Snura alisema kila mara mtoto wake anamuambia asikate tamaa ya kuwalea na kumuombea kwa Mungu, aweze kumsaidia ili waendelee kusoma na kupata huduma japo baba zao hawawajali yeye na mdogo wake kitu kinachomliza mara kwa mara.

“Yaani nasikiaga maumivu makali sana  mtoto wangu mdogo wa miaka sita tu ananiambia maneno hayo yananiumiza kuliko kitu chochote kile huwa yananifanya nijitahidi kila kukicha ili nisimuangushe na nitaendelea kukatika ili mtoto wangu apate elimu aitakayo,” alisema Snura ambaye amezalishwa watoto wawili na baba tofauti.

Wiki Moja Baada ya Ndoa, Masele Chapombe Amtongoza Upya Mke Wake


Loading...

Toa comment