The House of Favourite Newspapers

Mastaa Bongo wenye mashabiki wengi instagram

0

DIAMOND (2M)

Ni staa wa Bongo Fleva anayebamba na Ngoma ya  Make Me Sing. Diamond

anashikilia usukani kati ya  mastaa wa Bongo wenye mashabiki wengi ambao

ni zaidi ya milioni mbili (2,046,428).

WEMA (1.5M) 

Ni staa wa filamu Bongo. Wema Sepetu anashikilia nafasi ya pili akiwa na wafuasi zaidi ya  milioni moja na nusu (1,594,606).

MILLARD (1.5M) 

Ni mtangazaji maarufu nchini akimiliki pia studio yake binafsi ya kurushia  matangazo. Millard ambaye amejizolea  umaarufu kwenye mitandao na redio ana mashabiki zaidi ya milioni moja na nusu (1,577,345).

JOKATE (1.4M)

Mwanamitindo na Muigizaji, Jokate Mwegelo anasimama katika nafasiya nne akiwa na mashabiki

zaidi ya milioni moja na laki nne (1,497,197). Jokate

kwa sasa anamiliki lebo yake ya Kidoti inayojishusisha

na bidhaa za urembo.

WOLPER (1.4M)

Unaweza kumuita Wolper  Gambe. Mwanadada huyu ambaye ni mkali katika

tasnia ya uigizaji Bongo, ana mashabiki zaidi ya  milioni moja na laki nne

(1,476,933).

 VANESSA (1.4M)

Vee Money kama anavyojulikana katika  tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, naye ni miongoni

mwa mastaa wenye  mashabiki wengi akiwa na mashabiki zaidi ya milioni moja na laki nne (1,401,187).

SHILOLE (1.3M)

Ni staa wa Muziki wa Bongo Fleva pamoja na filamu. Shilole ama

Shishi amejizolea umaarufu kwenye nyimbo kama  Malele na Namchukua, ana

mashabiki wengi kwenye  mitandao ambao ni zaidi ya milioni moja na laki tatu. (1,377,428)

Leave A Reply