The House of Favourite Newspapers

MASTAA KONKI KWA PICHA CHAFU

MWILI ni kitu muhimu sana kinachotakiwa kuthaminiwa na kila binadamu. Huwezi kuwa mtu kamili kama huna mwili, hata vitabu vya dini vinatufundisha kwamba mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu hivyo siyo vyema kuuchafua au kuuacha kihasara.  

 

Kwenye ulimwengu wa mastaa, wao ni kama wamesahau kwamba mwili ni kitu cha thamani kwao kwani wapo ambao wamekuwa wakijiacha kihasarahasara kwa kukaa nusu utupu au kupiga picha za aibu ambazo licha ya kwamba ni kinyume na maadili ya Kitanzania, hata Mungu hapendi.

Katika makala hii tunaangalia baadhi ya mastaa ambao wamekuwa hawathamini kabisa miili yao na kama ingekuwa sheria inaruhusu wao kutembea uchi mtaani, huenda wangekuwa wanajitembeza tu maana ndivyo wanavyopenda.

 

SANCHI

Jina lake kamili ni Jane Rimoy ambaye ni mwanamitindo maarufu Bongo. Mwanadada huyu mwenye umbo matata linalomvutia kila mtu hasa wanaume wakware, anapenda sana kukaa nusu utupu. Amekuwa akipiga picha za kimitegomitego zinazomwacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake na kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii, hali inayowachefua wengi kwa kuwa siyo maadili.

 

Mwenyewe katika utetezi wake anadai amekuwa akipenda kukaa nusu utupu na kupiga picha hizo za kimitego ili apate fedha kwa kuwa anafanya uanamitindo, kitu ambacho anakipenda kutoka moyon i na siyo vinginevyo. “Ninapopiga picha hizi ni kazi kama kazi nyingine ya mitindo na wala sijiuzi kama watu wanavyonichukulia, lakini mbali na hivyo napenda tu,” alisema Sanchi.

AMBER LULU

Mwanamuziki Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ ni mmoja wa wadada ambao hawathamini miili yao kutokana na kujiachia kihasara kwa kukaa nusu utupu. Amber Lulu amekuwa akitupia picha za nusu utupu kwenye mitandao, hata akiwa anakatiza mitaani ni mtu anayependa kuvaa vikaptula au visketi vifupi vinavyomuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake.

 

Akiulizwa sababu za kupiga picha hizo hudai kuwa ni za matangazo ambazo zinamuingizia fedha kwani nyingi ni za kutangaza nguo za ndani na si kweli kwamba anajiuza. “Unajua watu wanaweza kukuchukulia ndivyo sivyo kwa sababu ya nguo au muonekano, mimi natangaza nguo za ndani jamani na ninapata mkwanja mrefu sasa niache nile wapi?” alihoji Amber Lulu.

SASHA

Muuza nyango kwenye video za wanamuziki wa Bongo Fleva, Sasha Kassim ‘Sasha’ licha ya kuwa na umbo zuri la kuwatoa udenda wanaume wakware, amekuwa akijiachia nusu utupu hasa mitandaoni.

 

Anaonekana kutouthamini kabisa mwili wake kama msichana mrembo na anapoulizwa husema kuwa picha hizo huwa anapiga kwa starehe yake, lakini pia zimebadilisha maisha yake kutokana na kupata dili mbalimbali, zimempa mchumba na umaarufu. “Ni picha zilizonipa umaarufu na faida kubwa, kwa sasa nimepunguza kidogo kutokana na Serikali kupiga marufuku na siyo kwamba nitaacha kabisa kwani nitajikuta nayumba kimaisha,” anasema Sasha.

GIGY MONEY

Licha ya kwamba msanii wa muziki Gift Stanford ‘Gigy Money’ ni mama wa mtoto mmoja, bado ameendelea kuacha mwili wake wazi kama alivyokuwa kabla ya kuwa mama.

 

Gigy amekuwa akivaa nguo zinazomwacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake na picha zake amekuwa akiziachia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Hata anapokuwa kwenye shughuli zake mitaani anapenda kuvaa nusu utupu. “Mimi sipo kwa ajili ya kiki, napenda kile ninachokifanya yaani kuvaa nusu utupu na ndicho ninachokifanya, nipo kwa ajili ya kutengeneza pesa tu,” alisema Gigy.

BABY MADAHA

Msanii huyu wa filamu na muziki Bongo ameingia kwenye listi hii kwa kuwa ni mwanadada anayependa kuacha nje matiti yake na kuvaa visketi na vikaptula vinavyoacha wazi sehemu kubwa ya mapaja yake.

Baby Madaha anasema tangu akiwa mdogo alipenda kuvaa nguo fupi, hivyo hata akiwa stejini anaimba hutamani kuvua nguo kutokana na mzuka wa kimuziki anaokuwa nao hivyo ‘kufuli’ kuonekana kwake siyo ishu. “Napenda fasheni na matiti yangu ni makubwa na yanavutia, jumlisha na mapaja yangu yamebana pia nina rangi nzuri, sasa kwa nini nijifunikefunike wakati jiji lenyewe la Dar joto!” Anasema Baby Madaha.

ISABELA MPANDA

Mwanamama huyu ni msanii wa Bongo Fleva ambaye ni mama wa watoto watatu, lakini amekuwa hajisitiri kama mwanamke au mama bali anauacha mwili wake wazi tu bila  kujali thamani yake. Isabela anapenda kuvaa nusu utupu kila anapoonekana, iwe nyumbani, mtaani au mitandaoni. “Kwanza Dar kuna joto sana pia nafurahi kuvaa nguo fupi kwa sababu nina miguu ya bia na sitaacha kuvaa hadi mwisho wa maisha yangu,” anasema Isabela.

QUEEN DARLEEN

Msanii wa Bongo Fleva, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ ni mama wa mtoto mmoja, lakini huwa hachagui cha kuvaa kwani mara nyingi huonekana akiwa amekaa nusu utupu akiwa na vikaptula na sketi fupi. Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Queen Darleen alisema anavaa hivyo kwa kuwa muziki wake ndiyo unaotaka hivyo na hawezi kupanda stejini akiwa amevaa baibui au kajitanda na ushung

Comments are closed.