The House of Favourite Newspapers

Mastaa wa taarab kuandika historia Dar live leo

0

MZEE-YUSUPH

MASTAA kibao wa Taarab wakiongozwa na Mzee Yusuf, Bi. Shakira, Khadija Kopa, Mwanahawa na wengine wengi, wanatarajia kuiandika historia mpya ya buradani kwa kuangusha bonge la shoo leo katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Juma Mbizo ambaye ndiye meneja wa ukumbi huo, amesema shoo hiyo itakuwa ya kihistoria kwa mwaka huu kwani ni ya kwanza kuwakusanya mastaa wengi wa Taarab katika jukwaa moja hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kupata burudani iliyoshiba.

“Itakuwa shoo baab’kubwa. We vuta picha Mzee Yusuf, Khadija Kopa, Hadija Yusuf, Joha Kassim, Mwanaidi Shaban kutoka Muungano, Shakira kutoka J.K.T, Mwanahawa na wengine kibao watakavyokuwa wanashusha nyimbo zao jukwaani. Patakuwa hapatoshi ni wimbo baada ya wimbo hadi usiku mnene,” alisema Mbizo.

Wakali wengine watakaolipamba jukwaa hilo chini ya udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Airtel ni pamoja na Sabaha Mchacho, Sihaba Juma, Hassan Soud, Thabit Abdul, Bi. Afua, Sizya Mazongela, Musta, Sihaba Juma na Zubeda Mlamali.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply