The House of Favourite Newspapers

MASTAA WAKABIDHIWA VIWANJA KIGAMBONI

WASANII mbalimbali wamenufaika na mpango wa kupatiwa viwanja na kulipa kidogokigodo kupitia Kundi la  Uzalendo Kwanza katika maeneo ya Kigamboni jijini Dar kupitia Kampuni ya KC LAND DEVELOPMENT PLAN Consultant Company Ltd.

Mbali na mastaa hao, kampuni hiyo inatarajia kutoa viwanja kwa wananchi ambao ni wanyonge na kwa kuwawezesha kulipa kidogokodogo.

Akizungumza na Global Publishers wakati wakikabidhiwa mkataba wa makubaliano kati ya kampuni hiyo na Uzalendo Kwanza katika Hoteli ya Lamada jijini Dar, Mwenyekiti wa Chama cha Uzalendo Kwanza Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ alisema kuwa amefurahi kuona kampuni hiyo imewachagua wanauzalendo kwanza kuwa miongoni mwa wanufaika wa viwanja hivyo na sasa kila mwanachama atamiliki kiwanja chake.

“Nawaomba wanauzalendo kwanza tutumie fursa hii ambayo itatufanya na sisi tuitwe baba na mama wenye nyumba, tumeona mpango kama huu kwa kundi la kina Joti ambao walipewa viwanja na sasa kila mmoja wao anamiliki majengo zaidi ya moja, binafsi nimeshapata kiwanja nitalipa kidokidogo mpaka nitakapomaliza chini ya utaratibu waliouweka,” alisema Steve huku akiwataka wananchi mbalimbali wachangamkie fursa kwa kuwaona KC LAND DEVELOPMENT PLAN Consultant Company Ltd.

 

Naye Mkurugenzi wa KC LAND DEVELOPMENT PLAN Consultant Company Ltd, Khalid Mwinyi alisema kampuni yao inayo viwanja ambavyo walianza kutoa kwa wananchi wa kawaida, sasa wamefuata na wasanii na baadaye yatafuata makundi mengine.

“Tumeanza na wananchi, wakafuata wasanii na baada ya hapo tutafata makundi mengine kwa mkopo usio kuwa na riba.

 

“Tuna viwanja maeneo tofautitofauti, ukiacha hivi vya Kigamboni, tunavyo pia mkoani Dodoma pamoja na Pwani ambavyo vyote tumepanga kuwapa wananchi kwa utaratibu mzuri na bei rahisi,” alisema Khalid.

Stori: Neema Adrian, Global Publishers

Comments are closed.