The House of Favourite Newspapers

MSAFARA WA MWILI WA DKT MENGI KUELEKEA LUGALO – VIDEO

SIMANZI, vilio na majonzi vimetawala kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakati wakiupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt Reginald Mengi ambao umeasili leo Jumatatu, Mei 6, 2019 nchini kutoka Dubai ambako umauti ulimkuta.

Maelfu ya wananchi walijipanga katika barabara za Jiji la Dar ambako mwili huo ulikuwa ukipitishwa na msafara kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere hadi katika Hospitali ya Lugalo ambako utahifadhiwa kabla ya kuagwa kesho na kuzikwa Alhamisi.

Wananchi hao waliokuwa na nyuso za huzuni huku wengi wao wakimwaga machozi kwa kukumbuka mema aliyokuwa akiyafanya hapa nchini ikiwemo kuwasaidia vijana, wazee, watu wenye ulemavu na makundi mbalimbali yenye uhitaji, jambo ambalo limeonekana kugusa wengi.

Aidha, mbali na kuonyesha huzuni zao, wananchi hao walizingira msafara huo na kuzia gari ili waeze kuuona mwili wa mzee Mengi na baada ya hapo walianza kulisukuma gari hilo kama ishara ya upendo wao kwa Mzee Mengi aliyekuwa nembo kubwa kwa taifa hususani katika kuwakwamua vijana na watu wasiojiweza.

 

PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL

TAZAMA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.