The House of Favourite Newspapers

Mastaa Wamiminika Uzinduzi wa Juice Kingdom Tabata, Usipime!

Mwanamuziki Q Boy Msafi, akiwa amepozi kwenye uzinduzi wa Juice Kingdom.

JANA, Tabata- Segerea jijini hapa kulikuwa na uzinduzi baab’kubwa wa kinywaji freshi ambapo Juice Kingdom, chini ya Mkurugenzi wake Zabron Julius walikuwa wanazindua tawi jipya.

Katika uzinduzi huo, mambo yalikuwa ni moto kwani mastaa mbalimbali waliibuka na burudani zilikuwa ni za kufa mtu.

Baadhi ya mastaa walioibuka ni muigizaji nguli Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, Blandina Chagula ‘Johari’, Salome Urasa ‘Thea’, David Genzi ‘Young Dee’, Abdulazizi Chende ‘Dogo Janja’ na mwanamuziki mwingine anayefanya vizuri kwa kasi na anajulikana kwa jina la Q Boy Msafi.

Mkali wa miondoko ya Singeli, Man Fongo akiwa kwenye pozi kwenye uzinduzi huo.

Hata hivyo mbali na wanamuziki hawa kutoa burudani na kuwasisitiza wakazi wa Tabata- Segerea kutumia juice maridhawa kutoka Kingdom, katika uzinduzi huo kila mtoto aliyekuwa maeneo hayo alipata juice bure.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Juice Kingdom, Zabron akizungumza na Wikenda alisema kwamba watengenezaji wa juice ni wengi lakini hakuna anayeshindana na Kingdom Juice.

Waigizaji Thea (kushoto), Johari (katikati) na Dude (kulia) wakifurahia juisi za Kingdom kwenye uzinduzi huo wa jana.

“Unajua juice zetu ni za kiwango cha juu sana, tunazingatia afya ya mwanadamu na tunamuandalia kiliocho bora. Kwa watu wenye kufahamu lakini hawazingatii ni kwamba juice ni matunda, na matunda ni muhimu kwa afya ya binadamu.

Mwanamuziki Young Dee akiwa amepozi na mshikaji wake kwenye uzinduzi huo (katikati).

“Sasa kuna watu unakuta kutokana na ubize wanashindwa kupata matunda wanayoyataka, sasa sisi Juice Kingdom tumewarahisishia watu, tunatengeneza juice za kila aina kwa hiyo badala ya mtu kuhangaika na matunda anaweza kupita akajipatia juis yake safi na maisha yakaendelea,” alisema Zabron.

Hata hivyo Zabron aliendelea kueleza kwamba tawi hilo la Tabata-Segerea ni moja kati ya matawi mengi ya Juice Kingdom na wanaendelea kuyafungua kutokana na namna watu wanavyofurahia juice za Kingdom.

Young Dee akiwa ameshika mkononi juisi kutoka Juice Kingdom.
Familia ya Mkurugenzi wa Juice Kingdom, Zabron Julius, ikiwa imetulia wakati uzinduzi ukiendelea.
Mkurugenzi wa Juice Kingdom, Zabron akiwa amembeba mwanaye Fame, kwenye uzinduzi huo wa tawi la Tabata Segerea.

 

Comments are closed.