KAJALA AWEKA NGUMU KUMUANIKA BABY WAKE
STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja ameweka ngumu kumuanika mpenzi wake wa sasa huku akirusha dongo kwa kusema kuwa, wanaotamani kumjua watahangaika sana.
Akipiga stori na gazeti hili, Kajala alisema, kuwa na mpenzi ni haki yake, lakini haoni kama kuna sababu ya kuufanya ulimwengu umjue maana kufanya hivyo kuna madhara yake. “Kama mwanamke ninaye anayenipa furaha, lakini siwezi kumuanika na wanaotamani kumjua watapata tabu sana. “Nimuanike ili iweje sasa? Nikimuanika nitawapa nafasi wabaya wangu kumpenyezea vitu vibaya kuhusu mimi na hatimaye kunitibulia hivyo watakaomjua ni ndugu zangu tu,” alisema Kajala.
STORI: Imelda Mtema, Dar
Comments are closed.