The House of Favourite Newspapers

Mastaa Yanga Wawekewa Bilioni 1.6 Kumuua Mwarabu Jumapili hii

0

IMEFAHAMIKA kuwa, mabosi wa Yanga wametenga bajeti ya Sh 1.6Bil kama bonasi kwa wachezaji wao kila watakapopata ushindi katika michezo ya hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Jumapili hii Yanga wanatarajiwa kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kundi D katika michuano hiyo ugenini dhidi ya US Monastir ya nchini Tunisia.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Olimpique Hammadi Agrebi huko Tunisia unaoingiza watazamaji 60,000.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, bajeti hiyo ya bonasi imewekwa kwa ajili ya kuwaongezea hamasa ya kupambana wachezaji ikiwa kwa viwango viwili.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kiwango cha kwanza kilichowekwa cha Sh 250Mil kwa kila mchezo watakaoucheza nyumbani na kupata ushindi watapewa kiasi hicho wachezaji na Benchi la Ufundi la timu hiyo.

Aliongeza kiwango kingine cha bonasi watakachopewa ni Sh 300Mil kwa kila mchezo watakaopata ushindi ugenini kwa kuanzia mchezo wa kwanza watakaocheza dhidi ya US Monastir huko Tunisia.

“Uongozi unataka kuona wachezaji wakipambana uwanjani na kufikia malengo, hivyo katika hatua hii ya makundi ya mashindano ya kimataifa, bajeti kubwa wamekewa wachezaji wetu kwa kila tutakapopata ushindi.

“Ipo hivi, kwa kila mchezo wa nyumbani ambao tutapata ushindi wa aina yoyote wachezaji wetu watapewa bonasi ya Sh 250Mil kwa lengo la kuwaongezea morali.

“Na kwa kila mchezo wa ugenini tutawapatia Sh 300Mil, viwango vimekuwa vya tofauti kutokana na umuhimu wa ushindi wa ugenini ambako pagumu kupata ushindi,” alisema mtoa taarifa huyo.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said hivi karibuni alizugumzia hilo la bonasi kwa kusema: “Bonasi ni siri kati ya mchezaji na mwajiri wake, hivyo ni ngumu kuweka wazi.”

STORI NA WILBERT MOLANDI | SPOTI XTRA

MASTAA YANGA WAWEKEWA BILIONI 1.6 KUMUUA MWARABU, SIMBA MIKAKATI MIZITO CAF | KROSI DONGO

Leave A Reply