The House of Favourite Newspapers

Maswali 10 Tata Kuvamiwa Kwa Kim Kardashian

PARIS, FRANCE - SEPTEMBER 30:  Kourtney Kardashian and Kim Kardashian West attend Buro 24/7 Fashion Forward Initiative as part  of Paris Fashion Week Womenswear Spring/Summer 2016 at Hotel Ritz on September 30, 2016 in Paris, France.  (Photo by Pascal Le Segretain/Getty Images for Buro 24/7)Kwa nini Kim na rafiki yake kipenzi, Simone Harouche walibaki chumbani wenyewe bila mlinzi wakati wakijua wana vito vyenye thamani kubwa na  kujipiga picha kisha kuzirusha kwenye mitandao ya kijamii?

kim-1Kwa nini awepo mlinzi mmoja tu kulinda  hoteli hiyo ya gharama  ambayo nyota wakubwa kama Madonna na Leonardo di Caprio hupanga? Nyumba hizo zina mpishi maalum, dereva na watumishi wengine.

kim-4Majambazi waliwezaje kuingia kwenye mlango wa hoteli hiyo wakati unalindwa na mitambo maalum. Milango haikuonyesha kama mtu alilazimisha kufungua au kuvunja kitasa.

Kwa nini hakukuwa na kamera za CCTV  katika nyumba hiyo ambayo ni ya gharama kubwa. Nyumba hiyo inalipiwa   karibu Sh 60milioni kwa wiki.

Ni taarifa gani mlinzi  aliyekuwepo lindo siku hiyo alikuwa nazo kuhusu Kim na wenzake hadi alipobanwa na kufungwa na majambazi akazitoa?

kim-5Kwa nini mlinzi wa Kim Pascal Duvier (kushoto) aliondoka na kumuacha mwanamitindo huyo peke yake. Majambazi walijuaje kuwa Kim yupo peke yake?

kim-6Kwa nini Kim aliruhusiwa kuondoka Ufaransa saa chache baada ya kuvamiwa?

Kwanini walinzi watatu pekee walipewa dhamana ya kumlinda Kim na ndugu zake kwenye kipindi hiki suala la ugaidi likiwa limeenea sana Ufaransa?

kim-2Kuna siri gani iliyojificha kuwezesha majambazi hao watano kuingia na kutoka ndani ya hoteli kisha kuondoka na pikipiki zao bila kutambulika wala kuonekana na mtu yeyote?

Kwanini hakuambiwa kuhusu usalama duni kwenye mitaa ya karibu na hoteli hiyo? Kama angeambiwa ni dhahiri angeweza kujilinda ama kwa kukodi walinzi zaidi.

Nani alaumiwe? Nani yuko nyuma ya mpango huu haramu?

Na Leonard Msigwa/MTANDAO.

 

 

Comments are closed.