The House of Favourite Newspapers

Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (Congenital Heart Diseases)

0

IDADI ya watoto wanaozaliwa wakiwa na matatizo ya moyo inazidi kuongezeka. Kwa bahati mbaya, ni wazazi wachache ambao huwa wanagundua mapema kinachowasumbua watoto wao na kujua nini cha kufanya ili kuokoa maisha yao.

Yapo matatizo mengi yanayohusisha ogani muhimu ya moyo, ambayo watoto huzaliwa nayo, kama ifuatavyo:

-Tundu kwenye moyo (septal defects)- Hali hii hutokea pale kunapokuwa na tundu kati ya upande wa kushoto wa moyo na upande wa kulia na kusababisha damu safi na chafu kuchanganyikana.

-Coarctation of the aorta – Hii ni hali ambayo hutokea pale mshipa mkubwa wa kusafirisha damu uitwao aorta unapokuwa mwembamba kuliko kawaida na kusababisha damu ishindwe kupita.

-Pulmonary valve stenosis- Hali hii hutokea pale valvu inayoratibu mzunguko wa damu kwenye chemba ya chini ya upande wa kulia wa moyo inayosukuma damu kupeleka kwenye mapafu, kuwa nyembamba kuliko kawaida.

-Kuungana kwa mishipa (transposition of the great arteries)- Hii ni hali ambayo hutokea pale mishipa ya pulmonary na artery inapoungana na kusababisha damu izunguke tofauti na utaratibu.

NINI HUSABABISHA?

Hakuna sababu za moja kwa moja zinazoelezea kwa nini watoto wengi huzaliwa wakiwa na matatizo ya moyo lakini tafiti zinaonesha kwamba baadhi ya mambo, huchangia tatizo hilo.

-Mama mjamzito anapokuwa anasumbuliwa na magonjwa ya vinasaba kama down’s syndrome, huwa kwenye hatari kubwa ya kuzaa watoto wenye matatizo ya moyo.

-Magonjwa mengine kama rubella, ni hatari kwa mjamzito na anapopata ni lazima atibiwe haraka kwani yakiachwa, husababisha mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo kwenye moyo.

-Ugonjwa wa kisukari kwa mama mjamzito, pia ni tatizo lingine linaloweza kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya moyo.

Kwa bahati nzuri, kama wazazi watakuwa makini, matatizo ya moyo ya mtoto huweza kuonekana kabla hata hajazaliwa kwa kutumia vipimo vya Ultra Sound. Tatizo linapogunduliwa mapema, huwa ni rahisi kupatiwa matibabu.

DALILI

Mtoto mwenye matatizo ya moyo, huwa na dalili zifuatazo:

-Mapigo ya moyo kwenda mbio.

-Kupumua harakaharaka hasa mtoto anaponyonya.

-Kutokwa sana na jasho.

-Mwili kukosa nguvu

-Rangi ya ngozi kubadilika. Dalili nyingine ni pamoja na mtoto kupoteza hamu ya kula, kuwa na uzito mdogo na kudumaa.

MATIBABU

Matatizo mengine

Baadhi ya matatizo, kama tundu kwenye moyo, huweza kutibiwa kwa dawa na taratibu tundu hujiziba lenyewe kadiri mtoto anavyokua mkubwa lakini lazima awe chini ya uangalizi.

Matatizo mengine huweza kutibiwa kwa upasuaji ambao ni lazima ufanywe na wataalam waliobobea, kwa bahati nzuri siku hizi matibabu ya moyo siyo lazima mgonjwa asafirishwe kwenda nje ya nchi, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inatoa matibabu. Muhimu ni kufuatilia kwa karibu afya ya mwanao ili kama kuna tatizo akapatiwe matibabu mapema.

Leave A Reply