The House of Favourite Newspapers

Mama Lulu Aitolea Povu Zito Ndoa Ya Mwanae

0
Staa wa sinema za Kibongo, Elizebeth Michael ‘Lulu’.

STORI: BRIGHTON MASALU | AMANI | HABARI

DAR ES SALAAM: Wakati kukiwa na madai ya kufanyika kwa vikao vya mwishomwisho vya harusi ya staa wa sinema za Kibongo, Elizebeth Michael ‘Lulu’, mama mzazi wa mrembo huyo, Lucresia Karugila ameitolea povu.
Mama Lulu aliliambia gazeti hili kuwa, hataki ujinga wa kuulizwaulizwa juu ya harusi hiyo badala yake aachwe ili apumzike nakufanya mambo ya msingi.

Mama mzazi wa mrembo huyo, Lucresia Karugila.

Hayo yalikuja kufuatia swali alilotwangwa na mwandishi wetu aliyetaka kujua juu ya maendeleo ya vikao vya harusi yamwanaye na mmiliki mmoja wa kituo cha redio na televisheni ambapo badala ya kutoa ufafanuzi,
alianza kumshambulia mwandishi wetu kwa maneno makali.
Mama Lulu alisema hataki kabisa kusikia jambo la ndoa wala mapenzi ya Lulu, kwani hakuna uhalali wala uthibitisho wa wazi alioupokea juu ya suala hilo, hivyo kumuuliza nini kinaendelea ni sawa na kumuingiza kwenye jambo la kijinga.
Mzazi huyo alimtahadharisha mwandishi wetu kuwa, asirudie kumtajia ndoa ya Lulu, kwani suala hilo linamsababishia kichefuchefu ambapo mahojiano kwa kifupi yalikuwa hivi;

Amani: Mama nataka kujua nini kinaendelea kwenye vikao vya mwisho vya harusi ya Lulu na ….(akitajiwa jina
la mchumba wa Lulu), wewe kama mama unasemaje?

Mama Lulu: Sitaki kabisa, kwanza una mama wewe? Sitaki kusikia ukinifuatilia na nilishakuambia tangu zamani, sitaki uniulize mambo ya kijinga kama hayo, hayanihusu kwa vyovyote, tena nisikusikie
kabisa, niache nifanye mambo yangu ya msingi, unasikia? Achana na mimi, tiiiii….titiiiiii (akakata simu).
Jitihada za kumpata Lulu kwa lengo la ufafanuzi juu ya jambo hilo la heri ziligonga mwamba kufuatia simu yake kutokuwa hewani hivyo jitihada bado zinaendelea.

Leave A Reply