The House of Favourite Newspapers

Matokeo Mabaya Kidato cha 6 Jangwani, Jafo Afanya Maamuzi Magumu

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ametaka uongozi wa shule ya Sekondari Jangwani kufanyiwa mabadiliko na kuwatoa walimu waliokaa zaidi ya miaka mitano wanaojiita ‘Wahenga wa Jangwani’ kufuatia matokeo mabaya ya shule hiyo kwa mtihani wa Taifa wa kidato cha sita.

Jafo ametoa maagizo hayo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar na kutoa siku moja yawe yametekelezwa kwani hajafurahishwa na usimamizi wa shule hiyo.

“Katika taaluma tunasema ninyi mna unyafuzi wa kitaaluma, katika shule yenu, matokeo yenu mabovu sana. Hivi inakuaje mtu uambiwe shule hii ina daraja la kwanza mmoja? Jangwani hali yenu ni mbaya”

“Jangwani Girls leo hii hakuna kitu, shule ambayo msichana popote pale Tanzania ndoto yake ni kusoma Jangwani, yenye upako maalum lakini leo inakua ya 3 kutoka mwisho, hii ni fedheha,” amesema Jafo.

Jafo amesema Shule hiyo ni miongoni mwa Shule chache zenye Walimu wengi lakini imekuwa katika kundi la mwisho.

“Shule ya Jangwani ina walimu 87, Shule ya Kibaha ina Walimu 52, yenye Walimu 52 inakua ya kwanza kitaifa lakini yenye Walimu 87 inakua ya tatu kutoka mwisho kitaifa,” alisema Jafo.

Comments are closed.