The House of Favourite Newspapers

Matokeo Ukonga, Makonda, Mambosasa Wafanya Haya – Video

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, RC Paul Makonda amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa ya kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kipindi chote cha kampeni za uchaguzi Jimbo la Ukonga hadi uchaguzi uliofanyika siku ya Jana na kumalizika salama pasipo uvunjifu wa amani.

Makonda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Askari katika Kituo Kikuu cha Polisi DSM (central) muda mfupi baada ya Matokeo kutangazwa na kuwataka waendelee kuwa majasiri kwani kazi yao ni ngumu na inahitaji uvumilivu wa hali ya juu.

Aidha RC Makonda amewapongeza wananchi kwa kulinda aman na kulifanya jiji la Dar es salaam kuzidi kuwa na amani masaa 24, huku akimpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Kamanda wa Polis Kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa kwa kuwa na vijana shupavu, wakakamavu na wenye morali ya kuwatumikia wananchi.

Kwa upande wake Kamanda wa Kanda Maalum ya DSM, Lazaro Mambosasa, amesema kuwa katika uchaguzi huo ambao Mwita Waitara (CCM) ameibuka mshindi, kikosi chake hakijatumia silaha ya aina yoyote sio risasi wala Bomu.

 

 

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.