The House of Favourite Newspapers

Matokeo Ya Kidato cha pili, Yapo Hapa

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk, Charles Msonde.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk, Charles Msonde leo Ijumaa Januari 4, 2019 amesema watahiniwa 506,235 walisajiliwa kufanya mtihani huo sawa na asilimia 92.87, kwamba wanafunzi 38,842 sawa na asilimia 7.13 hawakufanya mtihani kutokana na ugonjwa na utoro.

 

Amesema wanafunzi 452,273 sawa na asilimia 89.68 wamepata alama za ufaulu zitakazowawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

 

Amesema wanafunzi 52,073 sawa na asilimia 10.32 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha tatu.

 

Amesema mwaka 2017 wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 89.32 walipata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu, kwamba ikilinganishwa na 2018, ufaulu wa mwaka jana umeongezeka kwa asilimia 0.36.

Kutizama matokeo ya kidato cha pili >>>>> BONYEZA HAPA

Kutizama matokeo darasa la Nne >>>>> BONYEZA HAPA

Comments are closed.