The House of Favourite Newspapers

MAUA SAMA: IOKOTE IMENIACHIA ‘UCHIZI’

Related image
Maua Saleh ‘Maua Sama’

MSANII anayekimbiza kwenye gemu la Bongo Fleva, Maua Saleh ‘Maua Sama’ amesema kuwa licha ya wimbo wake mpya wa Iokote kutikisa kila kona lakini pia umemuachia ‘uchizi’.

Akizungumza na Mikito Nunusunusu, Maua aliyeimba wimbo huo kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu Banza Stone, Hanstone alisema kuwa, katika maisha yake hajawahi kutegemea kama ataachia wimbo wa kumchanganya kiasi hicho ambapo tangu autoe umezidi kumpa shoo hadi anachanganyikiwa.

“Yaani sijui hata nisemaje, Iokote imenifanyia maajabu makubwa sana hata nashindwa nielezeaje, kama huko nje ya nchi hadi sasa napata shoo hadi nachanganyikiwa nitajigawaje. Ukiingia mitaani, kwenye usafiri ndiyo nakuwa chizi kabisa,” alisema Maua.

Maua aliongeza kuwa, japo Iokote iliachiwa kwa kuvuja mitandaoni, zipo kolabo za kimataifa ameshazifanya ambazo atahakikisha hazivuji, kwani ni kali zaidi ya Iokote

STORI: Mikito Nunusunusu

Comments are closed.