The House of Favourite Newspapers

Maua Sama Naye Kufunga Jumla Jumla

BAADA ya wakali wa Hip Hop, Roma Mkatoliki na Stamina wanaounda Kundi la Rostam kuja na msemo wa Kufunga Jumlajumla, mkali wa R&B Bongo, Maua Sama naye ameunga msemo huo.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Maua anayetamba na Ngoma ya Iokote alisema ametokea kuvutiwa na msemo huo baada ya kuusikia na kwamba anatamani kuja na wimbo wenye jina hilo.

 

“Nimependa kwa kweli, kwa sababu msemo kama huu kutumika mwishoni mwa mwaka huwa mzuri, unaweza kukuta mtu umefanya biashara zako sasa unafunga jumlajumla ili ufungue mwaka mwingine.

“Nitajaribu kuongea na Rostam ikiwezekana nitatoka na wimbo wa Tunafunga Jumlajumla baada ya Iokote,” alisema Maua.

STORI: MWANDISHI WETU, DAR

BALAA LA GIGGY MONEY MOROGORO JUKWAA LA WASAFI FESTIVAL – VIDEO

Comments are closed.