The House of Favourite Newspapers
gunners X

Maua Sama, Ruby Kunogesha Siku Ya Urembo Asili

Msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama katika moja ya shoo yake iliyofanyika Dar Live

BAADA ya kusubiriwa kwa hamu na wajasiriamali na wadau wa urembo, hatimaye ile Siku ya Urembo wa Asili imewadia ambapo leo Jumamosi na kesho Jumapili kwenye Viwanja vya Life Park, Mwenge jijini Dar kutakuwa na bonge la burudani kutoka kwa wakali wa Muziki wa Bongo Fleva Maua Sama na Ruby.

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Ruby,

Mratibu wa tamasha hilo lenye kauli mbiu ya Nywele za Asili Siyo Ushamba ni Ujanja, Antu Mandoza, alisema kuwa, siku hiyo wasanii wengine watakaosindikiza siku hiyo kuanzia mapema saa mbili asubuhi ni Monalisa, Grace Matata na Mwasiti huku mgeni rasmi akiwa ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza.

“Kila kitu kimeshapangwa na tamasha litakuwa si la kitoto kwani kutakuwa na mabanda mengi ya wajasiriamali wa masuala ya urembo, pia ushauri na elimu ya bure utatolewa kwa wale wenye matatizo ya ngozi huku nikitoa banda moja kwa walemavu wajasiriamali,” alisema Mandoza na kuongeza.

“Pia kutakuwa na vitu vingi sana kama vile upimaji wa kansa, wajasiriamali na wakufunzi wa masuala ya urembo ambao siku hiyo watafundisha kutengeneza baadhi ya vitu ‘live’ kama vile Showergel.

 

“Kwa hiyo kama unajijua ni mjasiriamali wa mambo ya ngozi, nywele, msusi, hii ni fursa kubwa sana kwako kwani siku hiyo mbali na kuuza vipodozi, wahudhuriaji watapata fursa ya kujifunza urembo wa asili kupitia kwa madaktari wetu na timu ya ushauri.”

Comments are closed.