The House of Favourite Newspapers

Mauaji ya Kikatili Yamzeesha Mkuu wa Wilaya ya Njombe

0
Kissa Kasongwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe

MKUU wa Wilaya ya Njombe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Kissa Kasongwa ametangaza vita kwa mwananchi yeyote atakaye tekeleza mauaji kwa sababu mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi wilayani humo.

 

Kasongwa amesema tamaduni ya kuuana wilayani humo iwe mwisho kwa kuwa kuna mauaji ya kikatili hali inayoweza kusababisha watu wengine kuogopa kufika katika Wilaya hiyo.

 

“Tamaduni ya kuuana Njombe iwe mwisho,tumuombe Mungu atakase roho ya umauti inayozunguka kwenye hii Wilaya ya Njombe”alisema Bi,Kissa Kasongwa

Mkuu wa Wilaya akiongea na Wananchi wa Kata ya Iwungilo

Ameongez kuwa “Kuna mauaji ya kikatili Njombe mpaka nikasema duu! kwa umri mimi ni kijana lakini kwa mambo niliyoyapitia na kuyaona naona sasa nakaribia miaka 80”

 

Amebainisha haya wakati akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo katika Kata ya Iwungilo yenye lengo la kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.

Leave A Reply