The House of Favourite Newspapers

Mauzauza! Familia Zachapwa Bakola Usiku!

0

mauza uza (4)Wakazi wa Mtaa wa Kiyombo Shule, Nyantira Kata ya Kitunda jijini Dar, wakiwa kwenye kikao kujadili tukio hilo.

GLADNESS MALLYA Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Haya ni mauzauza jamani! Wakazi wa Mtaa wa Kiyombo Shule, Nyantira Kata ya Kitunda jijini Dar wamejikuta katika wakati mgumu kutokana na eneo hilo kutawaliwa na mauzauza ya kurushiwa mawe na kupigwa fimbo na watu wasioonekana hali inayowafanya washindwe kulala.
Akisimulia kwa masikitiko makubwa, mkazi mmoja ambaye ni mwathirika wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la mama Kasim alisema mawe hayo huanza kurushwa kwenye mabati juu ya nyumba kuanzia saa tatu usiku lakini wakitoka nje hawamuoni anayerusha na mawe pia.

mauza uza (2)

Viongozi wa Serikali ya Mtaa huo wakiongoza kikao.

“Ukweli tunateseka. Hatujui ni kitu gani kwani kuna kipindi yakianza kurushwa hivyo wote hapa nyumbani kwangu tunaugua miguu na kushindwa kutembea. Hapa mtaani kila mmoja na majanga yake, kuna wengine wanachapwa fimbo lakini wanaowachapa hawaonekani. Wakiamka asubuhi wanakuta wana alama za fimbo huku wamevimba.

“Wachungaji waliwahi kuja kuombea hapa kwenye nyumba ya jirani lakini walitoka nduki na kuacha kila kitu baada ya kurushiwa mawe na mrushaji haonekani,” alisema mama Kasim.

Kutokana na mauzauza hayo, mwenyekiti wa eneo hilo, Issa Chilemba wiki iliyopita aliitisha mkutano wa hadhara ambapo wakazi walijianika wanavyoteseka kwa kurushiwa mawe usiku na kushindwa kulala huku wengine wakieleza kuwa wakiamka asubuhi hujikuta wamechanjwa mwili mzima bila kujua ni nani anayewachanja.

mauza uza (3)

Kikao kikiendelea.

Pamoja na kurushiwa mawe na kuchanjwa wapo wengine walioeleza kuwa, walivuta umeme kwenye nyumba zao lakini uliwaka kwa siku moja na kuzima na walipoita mafundi hawakuona tatizo zaidi ya kugundua kwamba ni mambo ya kishirikina.

Katika mkutano huo, wananchi na mwenyekiti wao walikubaliana kuunda kamati ambayo itashughulikia suala hilo kwa kuchunguza wachawi wanaofanya mauzauza hayo, pia kuendelea kufunga na kumuomba Mungu kila mmoja kwa imani yake.

mauza uza (1)

Moja ya nyumba ya familia hizo.

“Kiukweli hili jambo ni la aibu na limenikera sana. Tunaweza kuleta mtaalam ‘sangoma’ hapa akawaumbua watu na heshima zao, hivyo nawaomba wanaofanya hivyo waache. Au kama kuna mtu anayedhaniwa kufanya hivyo naombeni mnipe jina lake kwa siri.

“Kupitia kamati hii maalum tunayounda ikipata majibu tutafanya maamuzi magumu ambapo atakayegundulika kwamba ndiye anayefanya mauzauza haya atahamishwa eneo hili,” alisema mwenyekiti huyo.

Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo, mwaka 2013 kulikuwa na tatizo kama hilo lakini waligundua kwamba ni kijana mdogo aliyekuwa akitumiwa kichawi na bibi yake ambapo walimrudisha kwao mkoani Njombe lakini Februari, mwaka huu mauzauza hayo yalianza tena.

Leave A Reply