The House of Favourite Newspapers

Mauzauza Yamhamisha Nyumba Gigy Money

Gift Stanford ‘Gigy Money’.

MAMBO juu ya mambo! Baada ya hivi karibuni kukabiliwa na msala wa picha za nusu utupu, sexy lady wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’, anadaiwa kuhama nyumba, kisa kutokewa na mauzauza.

 

Chanzo makini kilieleza kwamba, Gigy ambaye alikuwa akiishi Sinza- Kwaremi, Dar, hivi karibuni aliikimbia nyumba kwa kuwa kila akilala alikuwa akiona maruweruwe kama nyoka na mambo mengine ya ajabu hivyo kuamua kuhama.

 

“Gigy alikuwa anaona mambo ya ajabu sana kwenye nyumba aliyokuwa amepanga hivyo kutokana na hali hiyo akaamua kuhama kwa kuhofia kwamba yanaweza kumtokea makubwa zaidi na ikizingatiwa ana ujauzito kwa sasa,” kilieleza chanzo.

 

Alipoulizwa Gigy kuhusiana na hilo alikuwa na haya ya kusema: “Siyo kweli, nimehama kwa sababu niliona nyumba ndogo maana miezi michache ijayo nitakuwa mzazi hivyo ingekuwa vigumu sana kukaa kwenye nyumba hiyo.”

Risasi Vibes | RISASI MCHANGANYIKO

Comments are closed.