The House of Favourite Newspapers

Mavunde Azindua Programu ya KCB 2jiajiri Youth Scholarship

Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu kazi , Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (wa pili kushoto), akimkabidhi ruzuku ya gari aina ya kirikuu kwa Janeth Kipangula, mfanya biashara wa vifaa vya ujenzi wakati wa ambaye ni mmoja wa wanawake 256 ambao walipokea mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kupitia programu ya 2jiajiri. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa KCB Foundation, Bi. Jane Mwangi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Nd. Cosmas Kimario(kulia).
Mavunde (wa pili kulia), akimkabidhi ruzuku ya komputa na vifaa vingine nya ofisini kwa Bi. Halima Haji Sasya, ambaye ni mmoja wa wanawake 256 ambao walipokea mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kupitia programu ya 2jiajiri. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa KCB Foundation, Bi. Jane Mwangi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Nd. Cosmas Kimario(wa pili kushito).
Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya KCB 2jiajiri Youth Scholarship kwa wanafunzi wa Veta yaliyodhaminiwa na Benki ya Biashara ya KCB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya KCB, Cosmas Kimario, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya KCB 2jiajiri Youth Scholarship kwa vijana inayoendeshwa na VETA na kudhaminiwa na Benki ya KCB.

Comments are closed.