The House of Favourite Newspapers

MAYA AJIVUNIA MIAKA 20 BILA SKENDO

WAKATI akitimiza miaka 20 kwenye sanaa, mwigizaji ambaye ni tunda la Kundi la Kaole Sanaa, Mayasa Mrisho ‘Maya’ ameweka wazi kuwa, anajivunia miaka hiyo bila kukwaa skendo ambayo ingeweza kumshushia heshima kwenye kazi hiyo.

 

Maya aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, nidhamu hiyo ya kuheshimu kazi anayofanya walipata wasanii wa zamani ambao walikuwa wakisimamiwa kwenye vikundi na kuongozwa na wazee kama marehemu mzee Fundi Saidi ‘Kipara’ na Rajab Hatia ‘Pwagu’ ndiyo imemfanya kuepuka mambo ambayo yanaweza kumchafulia jina.

 

“Kiukweli hakuna kitu ambacho ninakiogopa kama skendo, lakini hiyo yote tulifundishwa zamani wakati tukiwa Kaole, ilikuwa ukifanya ujinga tu unaadabishwa na wazee,” alisema Maya.

Maya ni miongoni mwa wasanii wakongwe ambao walikuwa wakiunda Kundi la Kaole ambalo lilitoa waigizaji wengi wakali.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.