Maya: Mume Wangu ni Sapraiz

MAYAMUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa, watu wenye kiu ya kutaka kumjua mume wake mtarajiwa watulie watamuona tu na itakuwa sapraiz kwao.

 

Akizungumza na Amani, Maya ambaye tayari vikao vya harusi yake vimeshaanza, amesema mumewe mtarajiwa wametoka mbali na watu wengi wamekuwa hawamjui kutokana na aina ya maisha aliyojipangia.

 

“Mimi nimeishi maisha ya kujiheshimu na nimelelewa katika maadili ya kitanzania hivyo huwezi kujinadi na mpenzi, unamnadi mtu ambaye tayari ni mchumba au mume. Watu wasubiri tu watamuona mume wangu mtarajiwa,” alisema Maya.

Stori: Imelda Mtema

Toa comment