The House of Favourite Newspapers

Mayanja: Hans Poppe, Aveva msiniharibie timu

1

jackson-mayanja_16c1zw8tqege81g3qbstgngm9z

KOCHA wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja

Said Ally na Mohammed Mdose

KOCHA wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, ameutaka uongozi wa timu hiyo kutokiharibu kikosi cha sasa cha timu hiyo kwa kufanya mabadiliko makubwa kuelekea msimu ujao hata kama timu hiyo itafanya vibaya kwenye michezo ya mwisho na kukosa ubingwa.

Mayanja ametamka hayo wakati Simba ikiwa imebakiza michezo mitano kabla ya kumaliza ligi ambapo ujumbe huo unaonekana kumlenga mwenyekiti wa kamati ya usajili wa timu hiyo, Zacharia Hans Poppe ambaye ndiye ‘big boss’ kwenye masuala ya usajili, pamoja na rais wa timu hiyo, Evans Aveva.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mayanja amesema kuwa huo ni ushauri wake kwa viongozi hao kutokana na kikosi cha sasa kuonyesha kuelewa mbinu anazozifundisha, hivyo kama wakiletwa wachezaji wapya wengi itasababisha kuanza kufundisha upya, jambo ambalo litawachukua muda mrefu mpaka wao kumuelewa.

“Nawasihi viongozi kukiacha kikosi hiki na kutokiingilia hata kidogo mpaka msimu ujao, hata kama tutafanya vibaya kwenye michezo hii ya mwishoni mwa ligi na kujikuta tukipoteza ubingwa, japo siamini sana, maana tuna uwezo mkubwa wa kunyakua.

“Hiyo ni kwa sababu kama wakisajiliwa wachezaji wapya wengi, italazimu kuanza kufundishana upya ambapo mpaka wachezaji hao waweze kushika kila ambacho nitakuwa nawaelekeza, itatuchukua muda mrefu mpaka wao waje kufanya ninavyotaka na matokeo yake tunaweza tusifanye vizuri kama ambavyo nitabaki na kikosi kilichopo sasa,” alisema Mayanja.

1 Comment
  1. Hay Msham says

    Ni wazo zuri ukisemacho Mayanja ila ukiwa kama kocha inakubidi ukabiliane na hali yoyote utakayokutana nayo

Leave A Reply